Naibu waziri wa mazingira, tabianchi na wanyamapori wa Zimbabwe Bw. John Paradza, amesema Zimbabwe inapenda kuimarisha ushirikiano na China kuhimiza hifadhi ya wanyamapori na kufungua uwezo wa uchumi wake wa wanyamapori.
Bw. Paradza amesema Zimbabwe ina maliasili nyingi za bioanuwai, zinazotoa fursa nyingi kwa ushirikiano kati ya Zimbabwe na China.
Amesema wanaweza kuwa na wawekezaji zaidi walio rafiki kwa mazingira ambao wanaweza kushirikiana nao kuhimiza utalii wa wanyamapori, kwa sababu China ina soko kubwa.
Bw. Paradza amebainisha kuwa Zimbabwe inakabiliwa na changamoto kwenye uhifadhi wa wanyamapori, upungufu wa makazi na ongezeko la migongano kati ya binadamu na wanyamapori yanayotokana na kuongezeka kwa idadi ya wanyama wakubwa wanaokula majani.