Shirika la ndege la Kenya larejesha safari zake kwenda Msumbiji
2024-06-20 08:41:00| CRI

Shirika la Ndege la Kenya (KQ) limeanza tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Nairobi na Maputo ya Msumbiji ili kusaidia kuimarisha mawasiliano ya ndani ya Afrika.

Shirika hilo la kitaifa limesema safari hizo tatu za ndege kila wiki, Jumatano, Ijumaa, na Jumapili, zitahudumia wasafiri wanaotoka Kenya na zitatumika kama njia rahisi ya kuunganisha abiria kutoka miji mingine ya Afrika kupitia Nairobi.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Ndege la Kenya, Bw. Allan Kilavuka alisema kuzinduliwa upya kwa safari hizo ni udhihirisho wa wazi wa maendeleo ya shirika hilo na mustakabali mzuri.

Bw. Kilavuka alisema kuzinduliwa kwa njia ya 45 ya shirika hilo ya kwenda Maputo, kunaashiria hatua muhimu ya kampuni hiyo kupanua huduma zake.