Xi Jinping asisitiza utiifu wa kisiasa wa PLA katika mkutano uliofanyika mjini Yan’an
2024-06-20 13:56:37| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza utiifu wa kisiasa wa jeshi wakati wa mkutano wa kazi ya kisiasa wa jeshi uliofanyika mjini Yan'an, kambi ya zamani ya mapinduzi katika Mkoa wa Shaanxi kaskazini magharibi mwa China.

Akihutubia Mkutano wa Kazi ya Kisiasa wa Kamati Kuu ya Kijeshi CMC, uliofanyika Jumatatu hadi Jumatano, Xi Jinping ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi , ametaka zifanyike juhudi za kuleta uhakika kabisa wa kisiasa ili kujenga jeshi lenye nguvu.

Rais Xi amesisitiza haja ya kushikilia uongozi imara wa Chama jeshini na kujenga timu ya makada ya hali ya juu ambayo itakuwa na watu waaminifu, safi, wanaowajibika, na yenye uwezo wa kutimiza dhamira ya kuimarisha jeshi.