Kenya yazindua sensa ya wanyamapori ili kuboresha juhudi za uhifadhi
2024-06-20 22:58:25| cri

Kenya imezindua sensa ya wanyamapori itakayofanyika kwa mwaka mzima ambayo matokeo yake yataboresha miradi ya uhifadhi wa spishi za kipekee zinazopatikana nchini humo zinazokabiliwa na matishio ya hali ya hewa na shughuli za binadamu.

Sensa hiyo iliyozinduliwa jana na itakayofanyika kwa awamu, itaendelea mpaka mwezi Juni mwakani, na inalenga kutambua idadi kamili ya spishi zilizoko ardhini na baharini nchini humo.

Zoezi hilo linakuja wakati wanyamapori wanapungua kutokana na mgogoro kati ya wanyamapori na binadamu na ukame wa muda mrefu unaotokea katika mifumo yao ya ikolojia.

Waziri wa Utalii na Wanyamapori nchini Kenya Alfred Mutua amesema, zoezi hilo linalenga kutambua hali ya sasa ya idadi ya wanyamapori, tabia zao, na maeneo yao nchini humo.