Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Akili Bandia ya Mwaka 2024
2024-06-20 12:02:07| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda vya Akili Bandia ya Mwaka 2024.

Katika barua hiyo, rais Xi amesema akili bandia ni msukumo muhimu kwa duru mpya ya mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia na mageuzi ya viwanda, na italeta athari kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii duniani, na maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Amesema China inatilia maanani sana maendeleo ya akili bandia, na kufanya juhudi kubwa katika kuhimiza kuunganishwa kwa kina kwa mtandao wa Internet, Data Kubwa, Akili Bandia na uchumi halisi. Wakati huo huo, China inakuza viwanda vya akili bandia, na kuharakisha hatua ya kuendeleza Nguvu Mpya ya Uzalishaji, ili kutoa nguvu mpya kwa maendeleo ya hali ya juu. Pia amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani kuchukua fursa ya maendeleo ya kidijitali, mtandao wa Internet na akili bandia na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo na usimamizi wa akili bandia, ili kuhimiza maendeleo mazuri ya akili bandia, ukuaji wa uchumi duniani, na kuwanufaisha zaidi watu wote duniani.