Sehemu ya huduma za treni za abiria za reli ya TAZARA kuendelea
2024-06-20 08:41:39| CRI

Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) ilitangaza Jumatano kwamba treni za abiria zitaendelea kutoa huduma kati ya Dar es Salaam na Mbeya nchini Tanzania, na kati ya Kapiri Mposhi na Nakonde nchini Zambia.

TAZARA imesema katika taarifa yake kuwa mpango huu wa uendeshaji unatakiwa kufanyiwa mapitio zaidi, wakati TAZARA ikifanya kazi ya kutatua changamoto zilizopo na inalenga kurekebisha huduma zake za treni za abiria za kuvuka mpaka.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha TAZARA Bw. Conrad Simuchile, amesema baada ya juhudi za pamoja za kushughulikia changamoto za uendeshaji na mapitio ya kina ya hali inayowaathiri wasafiri, sehemu ya treni za abiria zitaendelea kufanya kazi. Tarehe 14 Juni, TAZARA ilitangaza kuwa shughuli za treni za abiria zingesitishwa kuanzia Juni 18 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.