Kenya inapanga kuwapa makazi mapya zaidi ya wakimbizi 700,000
2024-06-21 09:03:09| CRI

Kenya imesema itawapa makazi zaidi ya wakimbizi 700,000 kwenye sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya wadau wakuu kupitisha rasmi mpango wa kuwaingiza kwenye jumuiya za wenyeji.

Katibu mkuu wa Idara ya Taifa ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia Bw. Julius Bitok, alisema wadau wamepanga Mpango wa Shirika kuanza kutekelezwa na shirika hilo mwezi Novemba, ambao utasababisha kuundwa upya kwa kambi za wakimbizi katika kaunti za Garissa na Turkana kuwa manispaa.

Bw. Bitok amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi wakati wa kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, kwamba lengo la sasa ni kuhamasisha raslimali ili kutekeleza Mpango wa Shirika, huku awamu ya kwanza ya mradi wa miaka minne ikikadiriwa kugharimu dola milioni 943 za Kimarekani.