Watu wawili wamefariki dunia na wengine 47 wamelazwa katika vituo vya afya vilivyotengwa kutokana na kuambukizwa kipindupindu wiki iliyopita katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Masasi Loutery Kanoni amesema ugonjwa huo umeibuka katika kijiji cha Mbangala na alidokeza kuwa uhaba mkubwa wa maji ulioathiri sehemu kadhaa za Masasi unawezekana kuwa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya ya nchi hiyo, milipuko 134 ya kipindupindu katika maeneo 13 nchini humo imerekodiwa tangu tarehe 5 Januari mwaka huu ambapo watu 1,521 wameambukizwa na wengine 34 wamekufa.