Sudan Kusini yawasihi wakimbizi kujiunga na jamii zinazowapokea
2024-06-21 08:54:10| CRI

Sudan Kusini imewataka wakimbizi wajiunge na jamii zinazowapokea, ikiwa ni suluhu ya kudumu kwa msukosuko wa wakimbizi nchini humo.

Mkurugenzi mkuu anayeshughulikia ulinzi wa wakimbizi katika Kamisheni ya Mambo ya Wakimbizi ya Sudan Kusini Bw. Dut Akol Kuol amesema nchi hiyo kwa sasa inahifadhi wakimbizi 467,000 kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia na nchi nyingine, ambao ni vigumu kwa serikali kuwapatia makazi.

Ofisa huyo ametoa mwito kwa wakimbizi kujiunga na jamii kwenye maeneo walipo, badala ya kusubiri kupatiwa makazi ambayo hayatoshi kwa wote. Pia amewasihi wakimbizi kutoka Burundi na Ethiopia kurudi makwao kwa hiari kwa kuwa nchi zao kwa sasa ni tulivu.