Mjumbe maalum wa rais Xi Jinping wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Afrika Kusini
2024-06-21 09:23:27| CRI

Mjumbe Maalum wa rais Xi Jinping wa China Bw. Xiao Jie Jumatano alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini huko Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini.

Bw. Xiao Jie ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge la Umma la China amewasilisha pongezi na salamu za rais Xi kwa rais Ramaphosa, akisisitiza kuwa China inatilia maanani kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na inapenda kushirikiana na serikali mpya ya Afrika Kusini, kuongeza maelewano ya kisiasa, kupanua ushirikiano halisi na kusukuma ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Afrika Kusini ufikie ngazi ya juu zaidi.

Rais Ramaphosa amemshukuru Rais Xi kwa kutuma mjumbe maalum kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake.