Rais wa Malawi ateua makamu mpya wa rais
2024-06-21 11:01:52| cri

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemteua Michael Usi, Waziri wa Maliasili na Mabadiliko ya Tabianchi, kuwa makamu mpya wa rais wa nchi hiyo kufuatia kifo cha makamu wa rais Saulos Chilima kilichotokea Juni 10 kwa ajali ya ndege.

Rais Chakwera ametangaza uteuzi huo jana, ikiwa ni siku saba baada ya nafasi hiyo kuwa wazi, sawa na katiba ya Malawi inavyoelekeza.

Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri nchini Malawi imetangaza kuwa hafla ya kuapishwa kwa makamu mpya wa rais itafanyika leo mchana kwa saa za huko.