Vikosi vya RSF vyatangaza kuuteka mji wa serikali kusini mwa Sudan
2024-06-21 09:02:29| CRI

Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kimetangaza kuwa kimetwaa udhibiti wa mji wa kimkakati wa el-Fula, wa Jimbo la Kordofan Magharibi.

RSF kimesema katika taarifa yake kwamba "kimeudhibiti kikamilifu mji wa el-Fula, ambao una umuhimu wa kimkakati na ni mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Magharibi."

Shuhuda mmoja ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwamba makabiliano yalianza Jumatano kati ya RSF na vikosi vya Jeshi la Sudan (SAF) vilivyoko ndani ya kambi ya kijeshi nje kidogo ya mji huo. Amesema mapigano yalimalizika Alhamisi alasiri baada ya vikosi vya RSF kutwaa udhibiti wa kambi ya jeshi na kusambaza vikosi vyake katika mji mzima.