Xi asisitiza uhifadhi wa ikolojia na maendeleo ya hali ya juu ya bonde la Mto Manjano
2024-06-21 15:29:12| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza uhifadhi wa ikolojia na maendeleo ya hali ya juu ya bonde la Mto Manjano wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Ningxia Kaskazini Magharibi mwa China.

Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, alifika Ningxia Jumatano baada ya kukamilisha ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Qinghai.