Rwanda yapokea waangalizi zaidi ya 260 kusimamia uchaguzi ujao
2024-06-21 09:27:02| CRI

Tume ya uchaguzi ya taifa ya Rwanda (NEC) imetangaza kuwa imewapokea waangalizi 267 wa uchaguzi, wakiwemo 61 kutoka mashirika ya kimataifa, kwa ajili ya uchaguzi ujao wa rais na wabunge wa mwaka 2024.

Katibu mtendaji wa Tume ya NEC Bw. Charles Munyaneza amesema kwenye mkutano na wanahabari kuhusu maandalizi ya uchaguzi, kuwa mpaka sasa wamepokea waangalizi 267 wa uchaguzi na watapokea wengine zaidi hadi Julai 14.

Uchaguzi umepangwa kufanyika Julai 14 kwa wanyarwanda wanaoishi katika nchi za nje, Julai 15 kwa wale wanaoishi nchini Rwanda, Julai 16 kwa wajumbe wa makundi maalumu.