Mwanamitindo aliyenyolewa rasta gerezani apatwa na matatizo ya akili
2024-06-22 23:03:40| cri

Mwanamtindo wa mavazi maarufu nchini Uganda Bw Latif Madoi, amepatwa matatizo ya akili baada nywele zake ndefu (rasta) kunyolewa katika gereza la Kasangati.

Bw Madoi, 47, alikamatwa na polisi Mei 13 na wanafunzi wake wanne akiwa kwenye shule anayomiliki ya utaalamu wa mitindo. Alishtikiwa kwa kumiliki sare za wanajeshi na polisi kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za Uganda. Wakili wake Bw George Musisi alisema haamini mavazi hayo yalitoka kwenye shule ya mteja wake, akitaka polisi kuwasilisha ushahidi.

“Mteja wangu ana matatizo ya akili baada ya kukatwa nywele zake ndefu ambazo alitumia miaka 17 kuzikuza. Nywele hizo zilikuwa muhimu kwa utambulisho wake Bw Madoi,” alisema Bw Musisi.

Kukata nywele ni utaratibu wa kawaida kwa wafungwa wote nchini Uganda.