Watu 200 wajeruhiwa, 100 wakamatwa nchini Kenya kufuatia maandamano kupinga kodi
2024-06-24 10:55:04| cri

Watu 200 wamejeruhiwa na wengine 100 wamekamatwa nchini Kenya katika maandamano ya kundi la wanaopinga mifumo ya kodi nchini humo.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mtu mmoja ambaye hakujulikana jina amekufa katika Kituo cha Afya cha Blisa baada ya kupigwa risasi katika maandamano hayo, huku mtu mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 29 amefariki wakati akipatiwa matibabu katika kituo hicho Alhamisi iliyopita.

Waandamanaji hao wanapinga bajeti ya mwaka huu iliyosomwa hivi karibuni ambayo imelenga kuongeza kiasi cha Sh bilioni 2.7 kupitia kodi mbalimbali.

Waandamanaji hao wanadai watunga sheria wapige kura kupinga sheria ya matumizi ya serikali ambayo wanasema itakuwa mzigo kwa watumishi na wajasiriamali nchini humo.