Rais wa DRC aweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara za mizunguko unaofanywa na kampuni ya China
2024-06-24 10:55:58| cri

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi ameweka jiwe la msingi kwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za Kinshasa, moja ya miradi ya miundombinu inayopewa kipaumbele ndani ya fungu la ushirikiano la ‘rasilimali kwa miradi’ kati ya DRC na China.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi waandamizi, rais Tshisekedi amesema ana imani na ufundi wa Wachina, na kutaka kuwa na ushirikiano wa kina katika maeneo mengi kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Miundombinu na Kazi za Umma wa DRC Alexis Gisaro Muvuni amesema, mradi huo unaashiria ngazi mpya ya ushirikiano kati ya DRC na China ambao unaimarisha maingiliano ya barabara nchini humo.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini DRC Zhao Bin ameshukuru uungaji mkono wa DRC katika fungu la ushirikiano wa ‘rasilimali kwa miradi,’ akiuelezea mradi huo kama alama mpya ya Kinshasa na ishara mpya ya ushirikiano wa China na DRC katika sekta ya miundombinu.