FAO yapata mkataba wa dola za kimarekani milioni 25 ili kuboresha usalama wa chakula nchini Somalia
2024-06-24 09:39:30| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kwamba limetia saini mradi wa dola za kimarekani milioni 25 ili kuboresha usalama wa chakula na ustahimilivu nchini Somalia.

FAO imesema mradi huo unaoitwa TRANSFORM, ni sehemu muhimu ya Mpango mpana wa washirika mbalimbali wa Johwar Offstream Storage (JOSP). Mradi huo unalenga kukarabati miundombinu muhimu na kukuza kilimo kinachozingatia hali ya hewa kwa wakulima wadogo katika mji wa Jowhar jimboni Hirshabelle nchini Somalia.

Mwakilishi wa FAO nchini Somalia Etienne Peterschmitt amekaribisha ufadhili huo mpya na kusisitiza umuhimu wake katika kuchangia kuimarisha usalama wa chakula na ustahimilivu kwa jamii zilizo kando ya Mto Shabelle.