Saudi Arabia ilitangaza Jumapili kuwa imerekodi vifo 1,301 kati ya mahujaji wakati wa msimu wa Hijja, asilimia 83 kati yao walikuwa watu ambao hawajasajiliwa.
Shirika la Habari la Saudi liliripoti kuwa Waziri wa Afya wa Saudia Fahd Al-Jalajel alisema kuwa sekta ya afya ya nchi hiyo ilishughulikia kesi "nyingi" za shinikizo la joto, ambapo watu wengine bado wanapatiwa matibabu. Waziri huyo aliongeza kuwa miongoni mwa waliofariki walikuwemo wazee kadhaa na wagonjwa wa kudumu, akionesha kuwa joto liliathiri zaidi mahujaji ambao hawajasajiliwa kwani walitembea umbali mrefu wakipigwa na jua moja kwa moja bila ya kuwa na makazi ya kutosha au kupata utulivu.
Licha ya ukosefu wa taarifa binafsi au hati za utambulisho, wahanga wote wametambuliwa na familia zao zimearifiwa. Michakato inayofaa ilifuatwa wakati wa kuwatambua, maziko, na utoaji wa vyeti vya kifo.