Watu tisa, wakiwemo maafisa saba wa kutekeleza sheria, wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa kwa risasi kusini mwa Russia katika Jamhuri ya Dagestan siku ya Jumapili.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mashambulio hayo ya risasi yalitokea katika makanisa mawili ya kiorthodox, sinagogi na kituo cha polisi wa trafiki katika mji wa pwani wa Derbent na mji mkuu wa Dagestan wa Makhachkala.
Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi (NAC) imesema Kamati ya Uchunguzi ya Russia imefungua kesi za jinai chini ya kifungu kinachohusiana na shambulio la kigaidi juu ya mashambulizi hayo na operesheni ya serikali ya kukabiliana na ugaidi ilianzishwa huko Dagestan. Washambuliaji wanne waliohusika katika ufyatuaji risasi wameuawa na vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi zao.