IMF kuipa Tanzania dola za Marekani milioni 935.6
2024-06-24 22:54:08| cri

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) litaipatia Tanzania zaidi ya dola za Marekani milioni 935.6, sawa na shilingi trilioni 2.46 za Tanzania.

Taarifa ya uamuzi huo uliofikiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa IMF imetolewa hivi karibuni kupitia tovuti rasmi ya Shirika hilo, baada ya kumaliza mapitio ya tatu ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii kwa Tanzania.

Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 394.4 ni za kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania na shilingi trilioni 2.07 ni za kugharamia mpango wa miezi 23 wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Mfuko wa Unyumbufu na Endelevu (RSF).