Eneo la viwanda vya aluminiam linalofadhiliwa na China kukuza uchumi mseto wa Angola
2024-06-24 09:37:30| CRI

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Viwanda Carlos Rodrigues amesema eneo la viwanda lililowekezwa na China nchini Angola linatarajiwa kuunda mnyororo wa kina wa sekta, unaojumuisha utayarishaji wa aluminiam, uchanganuzi wa umeme na utengenezaji wa bidhaa za aluminiam, ambapo litakuza kwa kiasi kikubwa sekta ya taifa na kusaidia uchumi mseto.

Bw. Rodrigues ameeleza kuwa Mradi wa Eneo la Viwanda vya Aluminiam la Huatong, ulioendelezwa na muungano wa ‘Hebei Huatong Wire and Cables Group’ na Kiwanda cha Huatong cha Angola, utatekelezwa kwa awamu tano, huku ukiwekezwa kwa dola za Kimarekani bilioni 1.6. Aidha amesema uwekezaji huo mkubwa unaashiria hatua nyingine muhimu katika ajenda ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Angola na China, akiongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira 12,000.

Naye balozi wa China nchini Angola Zhang Bin alisema uwekezaji kama huo utaendeleza uchumi mseto wa Angola na ukuaji wa viwanda, kutoa ajira zaidi na mapato ya kodi, na kusaidia kutoa mafunzo kwa watu wenye vipaji vya kiufundi nchini.