Madhara ya matumizi ya Dawa za Kulevya kwa Vijana
2024-06-28 08:33:57| CRI

Matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa na madhara makubwa kwa vijana wanaojitumbukiza kwenye janga hili ni pia kuleta kikwazo kwa maendeleo endelevu ya binadamu. Ili kutambua umuhimu wa mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, tangu mwaka 1989, Jumuiya ya Kimataifa imekuwa ikiadhimisha Siku ya Kupambana na Biashara na Matumizi Haramu ya Dawa za Kulevya Duniani kila tarehe 26 Juni.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) inayohusika na Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inasema, lengo la siku hii ni kusaidia kuongeza uelewa mpana zaidi wa mapambano dhidi ya biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya duniani. Pia kushughulikia changamoto za dawa za kulevya katika majanga ya kiafya na kibinadamu. Hata hivyo jambo kubwa ambalo linaonekana kupuuzwa ni kuwasikiliza watoto na vijana, kwani hii ni hatua ya kwanza ya kupambana na hali hii ambayo imeendelea kuwasumbua vijana wengi duniani. Matumizi ya dawa za kulevya yana madhara makubwa kwa afya, maisha na jamii kwa ujumla hivyo lazima watu wote wapambane nayo. Kwa maana hiyo leo kwenye kipindi cha Ukumbi wa Wanawake tutajadili Madhara ya matumizi ya Dawa za Kulevya kwa Vijana.