Mke wa Rais Xi Jinping wa China Peng Liyuan, na mke wa Rais Andrzej Duda wa Poland, Agata Kornhauser-Duda, ambaye anafuatana na rais wa Poland katika ziara yake ya kitaifa nchini China, Jumatatu walitembelea Kituo cha Kitaifa cha Sanaa za maigizo cha China (NCPA) hapa Beijing.
Peng na Agata walitembelea vituo vya NCPA, na kutembelea maonesho ya sanaa kuhusu urithi wa kitamaduni usioshikika wa Beijing ambayo yanaonesha ufundistadi wa China.
Peng alisema China na Poland zinajivunia historia ndefu na mila za kitamaduni za kina. Mawasiliano kati ya watu na ya kiutamaduni kati ya pande hizo mbili yameongezeka zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Nchi hizo zikiboresha Zaidi mawasiliano ya kitamaduni, maelewano na urafiki kati ya watu wa pande mbili pia vitaimarishwa.
Peng na Agata waliangalia maonesho ya muziki wa jadi wa China, Opera ya Peking, na upigaji piano kutoka nchi zote mbili.
Naye Agata alisifu maonesho ya wasanii wa China, akisema kuwa utamaduni wa jadi wa China ni wa kushangaza na wa kuvutia. Alisema anatazamia mawasiliano na ushirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande mbili.