Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuboresha teknolojia ya sayansi na uvumbuzi katika kuifanya China kuwa ya kisasa na kuwa na maendeleo ya hali ya juu.
Rais Xi Jinping ameyasema hayo wakati alipotoa tuzo ya juu ya teknolojia ya sayansi ya China kwenye mkutano ulioshirikisha Mkutano wa teknolojia ya sayansi wa kitaifa, Mkutano wa taifa wa tuzo ya sayansi na teknolojia, na Mikutano Mikuu ya Wanataaluma wa Akadamia ya Sayansi ya China (CAS) na Akadamia ya Uhandisi ya China (CAE).
Rais Xi ametoa medali na vyeti vya tuzo ya juu zaidi ya teknolojia ya sayansi nchini kwa Li Deren msomi wa CAS na CAE kutoka Chuo Kikuu cha Wuhan, na msomi wa CAS kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua Xue Qikun, na baadaye kuwapongeza.