China kufanya mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya Kanuni Tano za Kuishi pamoja kwa Amani
2024-06-26 09:15:29| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Bi. Mao Ning amesema kuwa China itafanya Mkutano wa Kuadhimisha Miaka 70 ya Kanuni Tano za Kuishi pamoja kwa Amani Ijumaa mjini Beijing.

Miongo saba iliyopita, Waziri Mkuu wa wakati huo wa China Zhou Enlai alitoa kanuni hizi kikamilifu kwa mara ya kwanza, "kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa kila upande, kutodhulumiana, kutoingiliana mambo ya ndani, kuwa na usawa na kunufaishana, na kuishi pamoja kwa amani".

Ameongeza kuwa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zimekubaliwa na kutambuliwa na nchi zote duniani. Zimekuwa kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa wa kisasa na sheria ya kimataifa.

Wakati wa shamrashamra za maadhimisho ikiwemo kufanyika kwa mkutano mkuu wa maadhimisho, na vikao vingine mfululizo, Rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano mkuu wa maadhimisho na kutoa hotuba, na Waziri Mkuu Li Qiang ataongoza mkutano huo.