Afrika Kusini yaanza kuchunguza ugonjwa wa Mpox kwa wasafiri
2024-06-26 09:18:32| CRI

Mamlaka ya Usimamizi wa Mpaka ya Afrika Kusini (BMA) Jumanne ilisema imeanza uchunguzi wa ugonjwa wa Mpox kwa wasafiri wanaoingia nchini humo kwenye forodha zote kutokana na idadi ya kesi za maambukizi ya ugonjwa huo kuongezeka.

Kamishna wa BMA Michael Masiapato alitangaza kuwa maofisa wa afya wa forodha wameweka mpango kwa ajili ya kukabiliana na Mpox. Mpango wa sasa umeanza kutekelezwa kwa kuwa kesi 13 za maambukizi zimethibitishwa na idara ya afya ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa kamishna huyo, wasafiri wanapaswa kupimwa joto la mwili kwenye forodha za anga, barabara na bahari, na wasafiri wenye joto kali la mwili watawekwa karantini na kusaidiwa kuchunguzwa zaidi.