Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likilaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea katika Jamhuri ya Dagestan nchini Russia.
Taarifa hiyo imesema salamu za rambirambi zimetolewa kwa familia za wahanga wote, serikali na watu wa Russia, na kuwatakia waliojeruhiwa kupona haraka.
Likisisitiza kwamba aina na vitendo vyote vya ugaidi ni moja ya vitisho vikali kwa amani na usalama wa kimataifa, Baraza la Usalama limesisitiza haja ya kuwawajibisha wahalifu, waandaaji, na wafadhili wa vitendo hivi vya kulaumiwa vya kigaidi na kuwafikisha mbele ya sheria.