Mkuu wa jimbo la Gauteng asema serikali ya Umoja ya Afrika Kusini haitabadilisha sera zake
2024-06-27 09:00:50| CRI

Mkuu wa jimbo la Gauteng Panyaza Lesufi amesema kuwa sera ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini (GNU) haitabadilishwa.

Lesufi kutoka chama cha African National Congress (ANC) aliyasema hayo mjini Johannesburg katika mkutano wa kukuza ushirikiano wa kibiashara kati ya Beijing na Afrika Kusini. Tawi la Beijing la Baraza la Kukuza Biashara ya Kimataifa la China (CCPIT) liliongoza ujumbe wa jumuiya ya wafanyabiashara kwenda Johannesburg kutafuta fursa za biashara na ushirikiano na wenzao wa Afrika Kusini.

Ameongeza kuwa alipotembelea China, alifurahishwa na usalama wake ambao angependa kuona ukifanyika nchini Afrika Kusini. Afrika Kusini ipo kwenye mchakato wa kuijenga Johannesburg kuwa jiji la kisasa, akisisitiza ushirikiano na China utasaidia nchi hiyo kufikia lengo lake. Afrika Kusini inatazamia China kuboresha maendeleo ya miundombinu, treni za mwendo kasi na kukabiliana na uhaba wa nishati.