Mahakama Kuu ya Kenya yaamua jeshi lisaidie polisi kukabiliana na waandamanaji
2024-06-28 10:45:49| cri

Mahakama Kuu ya Kenya jana imehalalisha uamuzi wa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo (KDF) kusaidia Jeshi la Polisi kudumisha amani kufuatia maandamano ya kupinga mswada wa Fedha 2024/2025 yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na uharibifu mkubwa wa mali.

Jaji Lawrence Mugambi alikataa kuamuru askari wa KDF warudi katika kambi zao na kuwataka wazingatie sheria wanaposaidia polisi kudumisha amani chini ya uongozi wa Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Japhet Koome.

Wakati wa maandamano hayo ya siku tatu, maduka yaliporwa na biashara kusambaratishwa, huku watu zaidi ya 300 wakijeruhiwa wakati wa makabiliano ya waandamanaji na polisi katika kaunti 35 ambapo maandamano hayo yalifanyika.