Serikali ya Tanzania Alhamisi iliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ichukue hatua ili kukomesha mgomo wa siku nne uliofanywa na wenye maduka katika mikoa zaidi ya minane nchini humo.
Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika huko Dodoma msemaji mkuu wa serikali Thobias Makoba alisema, agizo hilo lilitolewa baada ya mkutano kati ya waziri mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wa vyama vya wafanyabiashara.
Makoba alisema TRA iliagizwa kusitisha ukaguzi wa risiti za kielektroniki kwa ajili ya ukusanyaji kodi, na kuacha kukusanya kodi kwa nguvu.
Wafanyabiashara katika mikoa minane Jumatatu walifunga maduka yao na kufanya mgomo kutokana na mrundikano wa kodi.