Zimbabwe inaelekea kumaliza mlipuko wa kipindupindu
2024-06-28 10:36:17| cri

Waziri wa Afya na Huduma za Watoto nchini Zimbabwe Douglas Mombeshora amesema, nchi hiyo inakaribia kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa kipindupindu ulioathiri mikoa yote 10, kama mwenendo wa sasa wa kupungua kwa kesi utaendelea.

Wizara hiyo imesema, watu 87 wamethibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo tangu mlipuko ulipotokea mwezi Februari mwaka jana.

Waziri Mombeshora amesema, baadhi ya mikoa haijaripoti kesi yoyote ya kipindupindu kwa zaidi ya mwezi mmoja, ambayo ni ishara nzuri kuwa nchi hiyo iko mbioni kumaliza mlipuko huo.

Amesema kama hakutakuwa na kesi yoyote kwa muda wa mwezi mmoja, nchi hiyo inaweza kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa huo,na kuongeza kuwa, kuna baadhi ya maeneo ambayo hakuna kesi zozote zilizoripotiwa katika wiki sita.