Maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula
2024-06-28 23:34:12| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, Sudan Kusini inakabiliwa na hali mbaya ya vurugu, mafuriko, na mgogoro wa uchumi na njaa, huku watu 79,000 katika mkoa wa Jonglei wakikabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.

Ofisi hiyo imesema zaidi ya watu milioni 7 nchini humo wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 20 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Ofisi hiyo imesema ongezeko hilo linatokana na uhaba wa fedha wa kujibu mahitaji ya kibinadamu na wakimbizi wapya wanaoingia nchini humo kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan.