Watu zaidi ya 18 wauawa katika milipuko ya kujitoa mhanga nchini Nigeria
2024-07-01 10:08:15| cri



Watu zaidi ya 18 wameuawa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika matukio matatu ya milipuko ya kujitoa mhanga iliyotokea jumamosi iliyopita kwenye jimbo la Borno nchini Nigeria.

Mamlaka ya kushughulikia mambo ya dharura ya jimbo la Borno imesema, washambuliaji wengi wa kujitoa mhanga walifanya mashambulio hayo kwa nyakati tofauti katika harusi, hospitali na mazishi, na hali ya majeruhi 19 ni mbaya.

Hadi kufikia sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na mashambulio hayo.