Tanzania yasema itasafirisha mahindi yenye thamani ya dola milioni 250 kwa Zambia iliyokumbwa na ukame
2024-07-01 14:36:36| cri

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Bw. Hussein Bashe amesema Tanzania itauza tani 650,000 za mahindi kwa Zambia, katika mpango wenye lengo la kusaidia nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kupunguza uhaba wa chakula unaosababishwa na ukame wa muda mrefu.

Bw. Bashe amesema nchi hizo mbili zimesaini makubaliano ya kusambaza nafaka hiyo, inayotarajiwa kulisha takriban watu milioni 7 nchini Zambia. Zambia inakabiliwa na ukame ambao umepunguza uzalishaji wa chakula na umeme, hivyo kushinikiza serikali kuagiza chakula kutoka nchi jirani. Makubaliano kuhusu biashara hiyo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ya Tanzania (NFRA) Bw. Andrew Komba, na mratibu wa taifa wa maafa wa Zambia Bw. Gabriel Pollen.