Jeshi la Sudan lakanusha taarifa za kikosi cha RSF kutwaa mji mkuu wa jimbo la Sinnar
2024-07-01 08:41:04| cri

Jeshi la Sudan (SAF) jumapili lilikanusha madai kwamba Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) kimechukua udhibiti wa Singa, mji mkuu wa Jimbo la Sinnar katikati mwa Sudan.

Katika taarifa yake, Msemaji wa Jeshi hilo Nabil Abdalla amesema, Singa imeshuhudia mapigano makali na uharibifu mkubwa wa mali za raia, huku kukiwa na ripoti za vifo vya raia.

Jumamosi jioni, msemaji wa RSF Bw. Al-Fateh Qurashi alitangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba, RSF inadhibiti kikamilifu mji wa Singa na inashikilia taasisi zote za jiji hilo, pamoja na makao makuu ya serikali ya jimbo.