Kabla ya ziara ya kiserikali ya rais Xi Jinping wa China nchini Tajikistan, shughuli ya kuonyesha vipindi vya televisheni vya CMG iliyoandaliwa kwa pamoja na CMG, shirika la habari la Khovar la Tajikistan, kituo cha televisheni cha Sinamo cha Tajikistan ilizinduliwa tarehe 30 Juni mjini Duschanbe, ambapo Vipindi zaidi 10 vitaonyeshwa kwenye vyombo vikuu vya habari vya nchini humo.
Mkuu wa kituo kikuu cha redio na televisheni cha China CMG Bw. Shen Haixiong, mhariri mkuu wa lugha ya kirussia wa shirika la habari la Khovar Bibi Elena Batenkova na balozi wa China nchini Tajikistan Bw. Ji Shumin wameshiriki na kuhutubia kwa njia ya video.
Bw. Shen Haixiong amesema, China na Tajikistan ni nchi zenye ujirani mwema, na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili ni wa enzi na dahari. Amesema Marais wa China na Tajikistan wamepanga mustakabali wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na pia wametoa fursa mpya kwa vyombo vya habari vya nchi hizo mbili kukuza urafiki na kuimarisha ushirikiano. Shughuli hiyo ni hatua nyingine ya kutekeleza matokeo ya mkutano kati ya marais hao wawili na kuimarisha mawasiliano kati ya nchi hizo mbili.