Rais wa Msumbiji afanya ziara Tanzania na kuhudhuria maonyesho ya Biashara ya Dar Julai 3
2024-07-01 14:34:37| cri

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imetangaza kuwa Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji atafanya ziara ya kiserikali ya siku 4 nchini Tanzania kuanzia Julai 1, kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Bw. January Makamba, amesema katika ziara hiyo Rais Nyusi atazindua Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) tarehe 3 Julai. Mbali na hayo yeye na mwenyeji wake pia watasaini makubaliano katika nyanja za afya, elimu na habari ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili.