Makubaliano mapya yaliyosainiwa kati ya Angola na China ni hatua kubwa katika ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili
2024-07-01 08:40:32| CRI

Msimamizi mtendaji wa Shirika la Uwekezaji Binafsi na Biashara ya nje ya Angola (AIPEX) Neide dos Santos amesema, makubaliano ya kukuza na kulinda uwekezaji kati ya China na Angola ambayo yalianza kutekelezwa Jumamosi, yataongeza uwezo wa Angola kuvutia uwekezaji wa kimkakati kutoka China, na pia ni hatua kubwa katika ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Santos amesema uwekezaji huo mkubwa utaleta ajira bora na mapato ya juu kwa makampuni na nchi ya Angola, na kwamba kwa sekta ya biashara, makubaliano hayo yanamaanisha soko tulivu lenye usalama zaidi kwa uwekezaji wa China. 

Makubaliano hayo yalisainiwa na Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio tarehe 6 Desemba mwaka 2023 mjini Beijing.