Rais Xi Jinping wa China leo adhuhuri amewasili Astana kwa ziara ya kiserikali nchini Kazakhstan, na pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) utakaofanyika nchini humo.
Mwanzoni mwa ziara hiyo, Rais Xi ametoa makala iitwayo “Tekeleza Kivitendo Azma ya Pamoja, Fungua Ukurasa Mpya wa Uhusiano kati ya China na Kazakhstan” kwenye gazeti la Kazakhstanskaya Pravda na shirika la habari la kimataifa la Kazakhstan.