Bidhaa zinazouzwa na Kenya zaruhusiwa kuingia kwenye soko la Umoja wa Ulaya bila ushuru
2024-07-02 09:27:23| cri



Kenya na Umoja wa Ulaya zimefikia hatua muhimu kwenye uhusiano wao wa kibiashara, na kuanza kutekeleza Makubaliano ya Wenzi wa Kiuchumi (EPA) jumatatu.

Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, Rebecca Miano, amesema kwenye taarifa yake kwamba, kwa mujibu wa EPA, bidhaa zote zinazouzwa na Kenya kwa soko la Umoja wa Ulaya sasa hazina ushuru na upendeleo, hatua itakayohimiza biashara ya bidhaa na kuimarisha uwekezaji kati ya pande hizo mbili.

Miano amesema Makubaliano ya EPA kati ya Umoja wa Ulaya na Kenya ni mojawapo ya makubaliano yenye matarajio makubwa, ambayo yanaweza kuwa mfano wa nchi nyingine za Afrika.