Naibu Katibu Mkuu wa UM: mkutano maalum wa tatu kuhusu suala la Afghanistan ni wazi na wenye manufaa
2024-07-02 10:43:39| cri

Mkutano maalum wa tatu wa siku mbili juu ya Afghanistan umemalizika. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kisiasa Bi. Rosemary DiCarlo amesema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano huo kuwa mkutano huo ni wazi na wenye manufaa.

Amesema wanatumia mbinu za kikanuni za hatua kwa hatua, ili kufahamu bayana matokeo yaliyopatikana na ahadi zilizotolewa. Ameongeza kuwa lengo la sasa ni kuwasiliana na pande zote za Afghanistan na kujadiliana na mamlaka ya utawala kuhusu mfululizo wa masuala muhimu. Zaidi ya hayo, Umoja wa Mataifa unafikiria kuanzisha kikosi kazi,  na kufanya mikutano ya vikundi kuhusu nyanja mbalimbali tofauti.