Watoto 9 wauawa katika shambulio lililofanywa na kikosi cha RSF magharibi mwa Sudan
2024-07-02 08:34:04| CRI

Watoto 9 wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio la anga lililofanywa na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) katika mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini, El Fasher, magharibi mwa Sudan.

Shirika lisilo la kiserikali la mjini El Fasher limesema, droni ya kikosi cha RSF ilidondosha makombora katika Msikiti wa Al-Hijra ulioko eneo la Al-Tijaniya mjini humo na kusababisha vifo na majeruhi hayo.

Wakati huohuo, gazeti la Sudan Tribunal limeripoti kuwa, sehemu iliyolengwa ni jiko ambalo linatumika kutoa chakula kwa watu wasio na makazi.

Kikosi cha RSF hakijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo.