Marais wa China na Kazakhstan wafanya mazungumzo Astana
2024-07-03 16:02:00| cri

Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev kwenye ikulu ya nchi hiyo mjini Astana.

Rais Xi amebainisha kuwa urafiki kati ya China na Kazakhstan ulikita mizizi kwenye njia ya kale ya hariri yenye historia ya zaidi ya miaka elfu moja, umekua kutokana na ushirikiano tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 32 iliyopita, na hadi sasa umefikia kiwango cha juu cha Uhusiano wa Kudumu wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote.

Rais Xi amesisitiza kuwa, haijalishi hali ya kimataifa itabadilika namna gani, nia ya China ya kulinda urafiki kati yake na Kazakhstan haitabadilika, azma yake ya kuendeleza ushirikiano na Kazakhstan haitabadilika, dhamira yake ya kuungana mkono kwenye masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya upande mwingine haitabadilika, na imani yake ya kutimiza malengo ya maendeleo ya kila upande haitabadilika.