Kundi la Houthi lafanya shambulizi tena dhidi ya Israel
2024-07-03 10:23:08| cri

Msemaji wa kundi la Houthi Yahya Sarea ametoa hotuba usiku wa tarehe pili mwezi huu akisema kundi hilo limefanya operesheni ya kijeshi dhidi ya shabaha muhimu mjini Haifa nchini Israel kwa makombora, likishirikiana na kundi la Islamic Resistance la Iraq.

Msemaji huyu ameongeza kuwa kundi la Houthi litaendelea kushirikiana na kundi hilo la Iraq kufanya operesheni za kijeshi za pamoja na kuwaunga mkono raia wa Palestina. Amesema kundi la Houthi halitasitisha operesheni husika hadi vita na vikwazo dhidi ya Palestina vitakaposimamishwa na kuondolewa.