Viwanda 25 kutoka nchini China vinashiriki maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba, kwa lengo la kuonyesha bidhaa wanazozalisha, kutengeneza mtandao na wafanyabiashara wa Tanzania na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kuwavutia wawekezaji Tanzania.
Miongoni mwa viwanda vilivyokuja ni pamoja na vya nguo, vifaa vya majumbani, simu, nishati ya jua, viatu, mitambo, vinywaji, Jenereta, magari, vyakula, na bidhaa za urembo, ambapo watatumia maonesho hayo kuuza na kuonesha bidhaa zao.
Mwandaaji wa maonesho hayo amesema baada ya kuona changamoto wanazopitia Wafanyabiashara wa Tanzania, vijana wa Tanzania waliosoma China waliona kuna haja ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na makampuni ya China kufanya biashara na kupata mizigo yao kwa wakati.