Watu 39 wauawa katika maandamano ya kupinga muswada wa nyongeza ya kodi nchini Kenya
2024-07-03 08:34:30| CRI

Watu 39 wameuawa na wengine 361 wengi kujeruhiwa katika maandamano ya hivi karibuni ya kupinga nyongeza ya kodi yaliyofanyika nchini Kenya, wakati vijana nchini humo wakiingia mtaani jana katika raundi mpya ya maandamano hayo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNHCR) Roseline Odede amesema katika taarifa yake iliyotolewa jumatatu jioni mjini Nairobi kuwa, takwimu hizo zinajumuisha kipindi cha kuanzia Juni 18 hadi Julai Mosi, na zinaonyesha kuwa jiji la Nairobi linaongoza kwa idadi ya vifo.