Tunisia yaandaa mkutano wa biashara na mataifa ya Afrika ili kukuza mauzo ya nje
2024-07-03 08:34:33| cri

Mkutano wa 3 ya Biashara kati ya Tunisia na Afrika ulianza jana jumanne katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, huku Tunisia ikilenga kuongeza mauzo yake ya nje kwa eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mkutano huo wa siku mbili ni sehemu ya juhudi za Tunisia kuongeza mauzo ya bidhaa kwa eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, na kukuza ujuzi wa Tunisia katika maeneo kadhaa, hasa katika sekta ya chakula, umeme, na dawa.

Biashara kati ya Tunisia na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara iliongezeka na kufikia dola za kimarekani milioni 650 mwaka jana, wakati mauzo ya Tunisia kwa nchi hizo yakizidi dola za kimarekani milioni 490, ikiwa ni sawa na asilimia 3.5 ya mauzo ya nje ya Tunisia.