Ofisa mmoja wa jimbo la Utter Pradesh, kaskazini mwa India amethibitisha kuwa, idadi ya waliofariki katika tukio la mkanyagano lililotokea jana Jumanne katika jimbo hilo imeongezeka na kufikia 116.
Amesema miili ya watu 88 ilikuwa imelazwa katika kituo cha watu waliojeruhiwa, 27 katika Hospitali ya Etah na mmoja katika hospitali katika mji wa Hathras.
Kulingana na ripoti za awali, karibu watu 50,000 walikuwa wamekusanyika katika mkutano wa kidini katika eneo la Sikandra Rao la Hathras, lakini kulikuwa na polisi 40 tu waliowekwa mahali hapo kusimamia umati huo.