Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuimarisha uratibu ili kupambana na ugaidi na msimamo mkali barani Afrika.
Katika ujumbe wake kwa njia ya video kweye Mkutano wa Jukwaa la Amani na Maendeleo Endelevu la Aswam, Guterres amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuunga mkono fursa ya Afrika kama kikapu cha chakula duniani na matakwa yake ya kuwa nguvu kubwa ya nishati ya kijani, huku ikihakikisha kuwa madini muhimu yanawanufaisha Waafrika kwanza.
Amesema jukwaa la Aswan linafanyika wakati Afrika iko katika wakati mgumu na dunia, kwa kuwa amani na maendeleo vinazuiwa na changamoto kubwa zinazoathiri Afrika na Waafrika kwa kiwango kikubwa.